PlaneteAfrique
Déconnexion

WS-Apps, Le système de gestion de contenu adaptatif développé depuis 15 ans est conçu pour sa puissance son efficacité et sa simplicité. WS-MySite! pour votre présence web immédiate, WS-Webzine pour vos publications, Ws-Ecommerce pour votre business.

Mbarali yaongoza kupata hati chafu ya matumizi nchini

Publié le 2/17/2014


Wilaya ya Mbarali imekuwa wilaya pekee nchini kupata hati chafu ya matumizi ya fedha kwa mwaka 2011/2012 kutokana na kukosekana kwa udhibiti wa ndani wa fedha zinazoletwa na serikali.



Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na kuwa hali hiyo inatokana na watendaji wa halamshauri hiyo pamoja na madiwani kushindwa kusimamia matumizi ya fedha katika miradi ya maendeleo ya wananchi.



KANDORO ametoa kauli hiyo wilayani Mbarali wakati wa kujibu hoja zilizowasilishwa na mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali-CAG, ambapo pamoja na mambo mengine halmashauri hiyo imeshindwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za matumizi ya fedha za umma zinazoelekezwa na serikali kwa wananchi.



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameendelea na ziara yake ya kushuhudia majibu ya hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa halmashauri sita kati ya kumi zilizopo mkoani humo na katika halamshauri ya wilaya ya Mbarali amekutana na hati chafu katika matumizi ya fedha za serikali na kutaja sababu zilizosababisha upatikanaji wa hati hiyo Chafu.



Pamoja na Wizara ya Utumishi kufanya uhakiki wa watumishi wote wa serikali mwaka 2011/2012, wilaya ya Mbarali inadaiwa kuendelea kulipa mishahara hewa kwa watumishi ambao wameshafariki dunia.



Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali Kenneth Ndingo amesema kupata hati chafu kwa halmashauri yake sio fedheha tu kwa wananchi wa mbarali badala yake ni aibu kwa mkoa mzima wa Mbeya.



Hosea Cheyo, TBC Mbeya.




Last Updated ( Wednesday, 11 September 2013 12:48 )


 


Continuer la lecture

TANZANIE - accès rapides

Actualités par pays

 

Newsletter


 
 
 
 
 
 

Actualités par pays

Newsletter


 
 
 
 
 

Pub GOOGLE

Tanzanie - Actualites