Mwakyembe aagiza matrekta bandarini kutumika kwa kilimo
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa miezi mitatu kwa watu wote walioingiza matrekta nchini ya kifungu cha msamaha wa kodi ili kuboresha kilimo nchini, wahakikishe zana hizo zinatumika kwa kazi hiyo na siyo vinginevyo.
Dkt. Mwakyembe ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya wakulima kwa nyanda za juu kusini yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale, huku akiagiza tabia ya kutumia matrekta kubeba na kukokota mizigo bandarini ikomeshwe mara moja na matrekta hayo yapelekwe mashambani kwa ajili ya kilimo.
Msimu wa maonesho ya wakulima na wafugaji umeanza, maonesho ya Nane nane kwa mikoa ya Kanda za Nyanda za Juu kusini yameshirikisha mikoa ya Njombe, Ruvuma, Katavi, Rukwa Iringa na Mbeya, mwaka huu maonesho haya yamezinduliwa na Waziri wa Uchukuzi Dtk. Harrison Mwakyembe.
Chama cha wakulima Nchini - TASO, Kanda ya Nyanda za Juu kusini kimepongeza hatua ya Waziri aliyofikia.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi amemhakikishia waziri mwaakyembe kuwa wako katika jitihada za kutumia vema ujio wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe, uwe ni manufaa kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya Nyanda za juu kusini.
Hosea Cheyo, TBC Mbeya.
Last Updated ( Friday, 02 August 2013 09:11 )