Polisi Tabora yasaka wapuuza usalama barabarani
Kutokana na ongezeko la ajali za barabarani zinazosababishwa na Wapanda baiskeli na Waendesha Pikipiki, Polisi mkoani Tabora imeanza oparesheni maalum ya kuwakamata watu wote wanaokiuka sheria za usalama barabarani.
Oparesheni hiyo inaenda sambamba na kutoa elimu ya sheria za usalama barabarani kwa Wapanda baiskeli, Waendesha Pikipiki na magari kwa lengo la kupunguza ajali za barabarani zinazosababisha vifo, ulemavu na uharibifu wa mali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi Peter Ouma amesema zoezi hilo ni endelevu mpaka hapo watakapojiridhisha kuwa hali ni shwari.
Nico Mwaibale, TBC Tabora.
Last Updated ( Friday, 21 June 2013 09:23 )