Mashirika kusaidia uboreshaji afya ya mama na mtoto
Mashirika ya kimataifa yanayotoa huduma za afya ya wazazi na mwana nchini yameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali mkoani Rukwa katika jitihada zake za kutoa tiba na kinga katika maeneo yote yenye miundombinu mibovu ya barabara, simu, ukosefu wa wataaalamu wa idara ya fya na uchache wa vifaatiba.
Mmoja wa wakurugenzi wa mashirika hayo ya Africare, Plan International na Jhpego bibi Sekai Chikomelo amesema vifo vingi vinavyotokea katika wilaya za Nkasi, Sumbawanga na Kalambo mkoani Rukwa vinatokana na ukosefu wa mbinu sahihi za kukabiliana navyo.
Akishiriki katika matukio ya kukabidhi magari mapya ya kuwahudumia wagonjwa maarufu kwa jina la ‘ambulance’ kwenye vituo vya afya vya Wampembe wilayani Nkasi na pia Mtowisa katika halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, bibi Chikomelo na bibi Wong wamesema kuwa mradi wa afya ya wazazi na watoto unalenga kupunguza idadi ya vifo vya akina mama wakati wa kujifungua kwa kuongeza vifaatiba, wataalamu na vyumba vya kupasulia.
Baadhi ya viongozi na wataalamu mkoani Rukwa wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Nkasi Idd Kimanta katibu tawala wa mkoa alhaj Salum Mohamed Chima na kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Rukwa Dr. Mtika walipata fursa ya kutoa nasaha zao juu ya umuhimu wa mazingira mazuri ya kukabiliana na maradhi.
Nswima Earnest, TBC Sumbawanga.
Last Updated ( Friday, 21 June 2013 09:26 )