Nape ashauri vyama vinavyovunja amani vifungiwe
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi - CCM itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amemtaka msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa kuvichukulia hatua za kisheria vyama vyenye usajili wa kudumu ambavyo vimekuwa vikisababisha uvunjifu wa amani.
Nnauye ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Njoro mkoani Kilimanjaro na kuongeza kuwa CCM haitavumilia kuona operesheni mbalimbali za vyama vya siasa hapa nchini zikiendeshwa bila kufuata taratibu.
Sauda Shimbo, TBC Kilimanjaro.
Last Updated ( Monday, 08 April 2013 11:26 )