Agakhan kujenga chuo Arusha
Mawaziri wanne wa wizara mbalimbali wametembelea eneo linalotarajiwa kujengwa chuo kikuu cha Agakhan mkoani Arusha kinachotarajiwa kukamilika mwaka 2018.
Katika ziara hiyo, Waziri wa elimu Dkt. Shukuru Kawambwa amesisitiza kuwa nchi ya Tanzania inakabiliwa na mahitaji makubwa ya vyuo vya elimu ya juu.
Dkt. Kawambwa ametoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea eneo litakalojengwa chuo hicho ambapo amesema iwapo chuo kikuu cha Agakhan kikikamilika kitakuwa na manufaa makubwa ndani na nje ya nchi na kuongeza kiwango cha ajira pamoja na kuipa sifa nchi ya Tanzania.
Sechelela Kongola, TBC Arusha.
Last Updated ( Monday, 08 April 2013 11:28 )