Watanzania waombwa kutunza amani
Viongozi na wafanyakazi wa mashirika mbalimbali walioshiriki kuwarejesha kwao wakimbizi wa Burundi waliokuwa wakihifadhiwa katika kambi ya Mtabila wilayani Kasulu wamewaomba watanzania kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuvuruga amani hapa nchini.
Wakizungumza baada ya kukamilisha kazi ya kuwarejesha kwao wakimbizi wa Burundi wamesema kuwa maisha ya ukimbizini waliyoyashuhudia ni ya shida na ghadhabu nyingi, hivyo watanzania wanapaswa kuhakikisha kuwa amani iliyopo nchini haipotei.
Baadhi ya viongozi wa serikali na wafanyakazi wa mashirika ya kitaifa na kimataifa wameshuhudia familia ya mwisho ya mkimbizi wa Burundi akipanda basi kurejea kwao.
Hata hivyo pamoja na mafanikio ya kukamilisha kazi ya kuwarejeshwa kwao zaidi ya wakimbizi elfu 35 kabla ya muda uliopangwa walikabiliwa na changamoto mbalimbali wakati wa utekelezaji wa kazi yenyewe.
Moja ya changamoto ilikuwa ni baadhi ya wakimbizi kukataa kupanda mabasi kwa kuhofia usalama wao huko waendako, hali iliyolazimu mbinu za ziada kuwashawishi kutumia.
Ili kuepuka machafuko, mkuu wa wilaya ya Kasulu Dany Makanga, viongozi na watumishi wengine wametoa raia kwa Watanzania kudumisha amani, utulivu na upendo miongoni mwao.
Wakizungumza eneo la Musenyi nchini Burundi Lewisi Kisanja na John Claudio waliokuwa wakisubiri kwenda maeneo ya mikoa yao ya kuishi wameiomba serikali yao ya Burundi kuwalinda, kuwaendeleza kielimu na kuwapatia maeneo ya Kilimo.
Dotto Elias. TBC Kigoma.
Last Updated ( Thursday, 13 December 2012 11:33 )