Skauti wasafisha eneo la TBC Mwanza
Wiki ya skauti duniani inayofikia kilele chake februari 22 ya kila mwaka imeadhimishwa katika wilaya ya ilemela mkoani mwanza kwa wanachama wa chama cha skauti wilayani humo kufanya usafi wa mazingira katika eneo la kituo cha shirika la utangazaji Tanzania (TBC)kituo cha mwanza.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo la usafi wa mazingira kamishna wa skauti wilaya ya ilemela Haji Jumanne ametoa wito kwa vijana nchini kujenga tabia ya kufanya kazi mbalimbali za kujitolea ikiwemo usafi ili kuondoa baadhi ya kero zinazowakabili wananchi.
Zoezi hilo la usafi wa mazingira lilifanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya skauti duniani inayoadhimishwa kila ifikapo februari 22 ya kila mwaka.
Kamishna wa skauti wilaya ya ilemela Haji Jummane ameelzea changamoto wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao kuwa ni pamoja na ukosefu wa usafiri na fedha.
Amicus Butunga, TBC Mwanza.
Last Updated ( Friday, 22 February 2013 11:25 )