CRDB yatoa zawadi za krismasi kwa wagonjwa Lindi
Benki ya CRDB Tawi la mkoa wa Lindi imetoa vyandarua hamsini pamoja na vinywaji mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya mkoa huo ya Sokoine ikiwa ni kuungana nao katika kusherehekea sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya.
Akikabidhi zawadi hizo ikiwa ni pamoja na vyandarua kwa watoto na akina mama wajawazito, sabuni, maji, soda,juisi na vinginevyo, Afisa wa Benki ya CRDB mkoa wa Lindi Abdallah Mohamed amesema ni kawaida ya benki hiyo kufanya hivyo kwa jamii kutokana na faida wanayoipata.
Kwa upande wake, muuguzi msaidizi wa hospitali hiyo Marieta Ng’oge ametoa shukrani kwa Benki ya CRDB na kuomba taasisi zingine kuiga mfano huo.
Kwa upande wao wagonjwa nao wameshukuru na kusema wamejiona ni watu waliojawa na furaha kwani sio kawaida mtu kuacha kufanya shughuli zake na kwenda kuwaona wao.
Martina Ngulumbi, TBC Lindi.
Last Updated ( Monday, 24 December 2012 13:14 )