DC Nachingwea awataka wazazi kuchangia elimu
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Regina Chonjo amewataka wazazi wilayani humo kuchangia elimu ya watoto wao kwa kuwalipia ada, kununua sare za shule na kufuatilia kwa karibu maendeleo ya masomo yao.
Chonjo amesema hayo kwenye mahafali ya pili ya shule ya awali ya Kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Nachingwea na kuongeza kuwa ukimsomesha mtoto wa kike ni kufungua ukurasa mpya wa maendeleo katika nchi.
Kwa upande wake Paroko wa Kanisa hilo, Fabian Ng’ombo amesema shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundombinu.
Martina Ngulumbi, TBC Lindi.
Last Updated ( Thursday, 13 December 2012 11:36 )